Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alizungumza nao kupitia kwa mkalimani.
Hagai 2:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Niliwapiga kwa ukavu, na ukungu, na mvua ya mawe, katika kazi zote za mikono yenu; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Niliwapiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, nikaharibu kila mlichojaribu kupanda, lakini hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Niliwapiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, nikaharibu kila mlichojaribu kupanda, lakini hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Niliwapiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, nikaharibu kila mlichojaribu kupanda, lakini hata hivyo hamkunirudia. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kazi zenu zote za mikono nilizipiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, lakini hata hivyo, hamkunigeukia mimi,’ asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kazi zenu zote za mikono nilizipiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, lakini hata hivyo, hamkunigeukia mimi,’ asema bwana. BIBLIA KISWAHILI Niliwapiga kwa ukavu, na ukungu, na mvua ya mawe, katika kazi zote za mikono yenu; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA. |
Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alizungumza nao kupitia kwa mkalimani.
Mmoja wao alipofungua gunia lake ili ampe punda wake chakula katika nyumba ya wageni, aliiona fedha yake; kumbe! Iko kinywani mwa gunia lake.
Naye Yusufu alikuwa ni mkuu juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.
Ikiwa kuna njaa katika nchi, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewazingira katika mji wao wowote ule; au ukiwapo msiba wowote, au ugonjwa wowote;
Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukame, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao, au ukiwapo msiba wowote, au ugonjwa wowote;
Tazama, Bwana ana mmoja aliye hodari, mwenye nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe, tufani iharibuyo, kama dhoruba ya maji mengi yafurikayo, ndivyo atakavyotupa chini kwa mkono.
Ndiyo sababu wenyeji wao wakawa hawana nguvu, na kufadhaika, na kuhangaika, wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya madari, kama shamba la ngano kabla haijaiva.
Kwa sababu hiyo alimwaga ukali wa hasira yake juu yake, na nguvu za vita; ukawasha moto wa kumzunguka pande zote, wala hakujua; ukamteketeza, wala hakuyatia hayo moyoni mwake.
BWANA ameapa kwa mkono wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.
Lakini kitu cha aibu kimeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu; makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.
Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono.
Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.
Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha mbali. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu yumba yangu imebaki kuwa gofu la nyumba, wakati ambapo kila mmoja wenu anakimbilia nyumbani kwake.
katika wakati huo wote, mtu alipofikia rundo la vipimo ishirini, palikuwa na vipimo kumi tu; na mtu alipofikia pipa kubwa apate kuteka divai ya vyombo hamsini, palikuwa na divai ya vyombo ishirini tu.
Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.
BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa joto jingi, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.