Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.
Hagai 1:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndio maana mbingu zimeacha kunyesha mvua, nayo ardhi haioteshi mavuno. Biblia Habari Njema - BHND Ndio maana mbingu zimeacha kunyesha mvua, nayo ardhi haioteshi mavuno. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndio maana mbingu zimeacha kunyesha mvua, nayo ardhi haioteshi mavuno. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo, mbingu zimezuia umande wake na ardhi mavuno yake kwa sababu yenu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo, kwa sababu yenu mbingu zimezuia umande wake na ardhi mavuno yake. BIBLIA KISWAHILI Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake. |
Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.
Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, wakati ule utakapowatesa;
Basi kwa ajili ya hayo, nitaitwaa tena ngano yangu kwa wakati wake, na divai yangu kwa wakati wake, nami nitamnyang'anya sufu yangu na kitani yangu, vya kumfunika uchi wake.
Nami nitakivunja kiburi cha uwezo wenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa kama shaba;
Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.