Basi, angalieni, na kuvitunza vitu hivi, hata mtakapovipima mbele ya wakuu wa makuhani, na Walawi, na wakuu wa koo za mababa wa Israeli, huko Yerusalemu, katika vyumba vya nyumba ya BWANA.
Ezra 8:34 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC vile vyombo vyote kwa hesabu na kwa uzani; tena uzani wake wote uliandikwa wakati ule. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila kitu kilihesabiwa na kupimwa na wakati huo uzito wa kila kitu uliandikwa. Biblia Habari Njema - BHND Kila kitu kilihesabiwa na kupimwa na wakati huo uzito wa kila kitu uliandikwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila kitu kilihesabiwa na kupimwa na wakati huo uzito wa kila kitu uliandikwa. Neno: Bibilia Takatifu Kila kitu kilihesabiwa kwa idadi na kupimwa kwa uzito, nao uzito wote uliandikwa wakati ule. Neno: Maandiko Matakatifu Kila kitu kilihesabiwa kwa idadi na kupimwa kwa uzito, nao uzito wote uliandikwa wakati ule. BIBLIA KISWAHILI vile vyombo vyote kwa hesabu na kwa uzani; tena uzani wake wote uliandikwa wakati ule. |
Basi, angalieni, na kuvitunza vitu hivi, hata mtakapovipima mbele ya wakuu wa makuhani, na Walawi, na wakuu wa koo za mababa wa Israeli, huko Yerusalemu, katika vyumba vya nyumba ya BWANA.
Hata siku ya nne, hizo fedha na dhahabu na vile vyombo vilipimwa ndani ya nyumba ya Mungu, vikatiwa mikononi mwa Meremothi, mwana wa Uria, kuhani; na pamoja naye alikuwapo Eleazari, mwana wa Finehasi; na pamoja nao Yozabadi, mwana wa Yeshua, na Noadia, mwana wa Binui, Walawi;
Na wana wa uhamisho, waliokuwa wametoka katika uhamisho wakamtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa, ng'ombe kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, na kondoo dume tisini na sita, na wana-kondoo sabini na saba, na mabeberu kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi, hao wote pia walikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.