Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Ezra 7:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa baba zetu, aliyetia neno kama hilo katika moyo wa mfalme, kuipamba nyumba ya BWANA iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ezra akasema, “Na asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zetu; ambaye amempatia mfalme moyo wa kutia mapambo nyumba ya Mwenyezi-Mungu iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ezra akasema, “Na asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zetu; ambaye amempatia mfalme moyo wa kutia mapambo nyumba ya Mwenyezi-Mungu iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ezra akasema, “Na asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zetu; ambaye amempatia mfalme moyo wa kutia mapambo nyumba ya Mwenyezi-Mungu iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zetu, Mungu ambaye kwa njia hii ameweka ndani ya moyo wa mfalme kuipa heshima nyumba ya Mwenyezi Mungu iliyo Yerusalemu, kwa namna hii

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Sifa ziwe kwa bwana, Mungu wa baba zetu, Mungu ambaye kwa njia hii ameweka ndani ya moyo wa mfalme kuipa heshima nyumba ya bwana iliyoko Yerusalemu, kwa namna hii

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa baba zetu, aliyetia neno kama hilo katika moyo wa mfalme, kuipamba nyumba ya BWANA iliyoko Yerusalemu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Ezra 7:27
16 Marejeleo ya Msalaba  

Hata walipokuja Hezekia na wakuu, na kuyaona yale mafungu, wakamhimidi BWANA, na watu wake Israeli.


wakaifanya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu kwa furaha, kwa muda wa siku saba; kwa kuwa BWANA amewafurahisha, na kumgeuza moyo mfalme wa Ashuru, awaelekee, ili awatie nguvu mikono yao katika kazi hiyo ya nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli.


Kisha nikaondoka usiku, mimi pamoja na watu wachache; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe.


nipewe na waraka kwa Asafu, mwenye kuutunza msitu wa mfalme, ili anipe miti ya kutengenezea boriti kwa malango ya ngome ya hekalu, na kwa ukuta wa mji; na kwa nyumba ile nitakapoishi mimi. Naye mfalme akanipa, maana mkono mwema wa Mungu wangu ulikuwa juu yangu.


Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na maofisa, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;


Musa akamwambia Farao, Haya, ujitukuze juu yangu katika jambo hili; sema ni lini unapotaka nikuombee wewe, na watumishi wako, na watu wako, ili hao vyura waangamizwe watoke kwako wewe na nyumba zako, wakae ndani ya mto tu.


Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.


Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, Mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; Ili kupapamba mahali pangu patakatifu, Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.


maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi.


Lakini ahimidiwe Mungu atiaye bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.


Nilifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.


Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika fikira zao nitaziandika; ndipo anenapo,


Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika fikira zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.


Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.