Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri watunza hazina wote, walio ng'ambo ya Mto, ya kwamba, kila neno ambalo Ezra, kuhani, mwandishi wa Torati ya Mungu wa mbinguni, atalitaka kwenu, na litendeke kwa bidii nyingi,
Ezra 7:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC hata kiasi cha talanta mia moja za fedha, na vipimo mia vya ngano, na bathi mia moja za divai, na bathi mia moja za mafuta na chumvi ya kiasi chochote kile. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema fedha kiasi atakacho mpaka kufikia kilo 3,400, ngano kilo 10,000, divai lita 2,000, mafuta lita 2,000, na chumvi kiasi chochote atakachohitaji. Biblia Habari Njema - BHND fedha kiasi atakacho mpaka kufikia kilo 3,400, ngano kilo 10,000, divai lita 2,000, mafuta lita 2,000, na chumvi kiasi chochote atakachohitaji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza fedha kiasi atakacho mpaka kufikia kilo 3,400, ngano kilo 10,000, divai lita 2,000, mafuta lita 2,000, na chumvi kiasi chochote atakachohitaji. Neno: Bibilia Takatifu talanta mia moja za fedha, ngano kori mia moja, divai bathi mia moja, mafuta ya zeituni bathi mia moja, na chumvi kiasi chochote. Neno: Maandiko Matakatifu talanta 100 za fedha, ngano kori 100, divai bathi 100, mafuta ya zeituni bathi 100, na chumvi kiasi chochote. BIBLIA KISWAHILI hata kiasi cha talanta mia moja za fedha, na vipimo mia vya ngano, na bathi mia moja za divai, na bathi mia moja za mafuta na chumvi ya kiasi chochote kile. |
Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri watunza hazina wote, walio ng'ambo ya Mto, ya kwamba, kila neno ambalo Ezra, kuhani, mwandishi wa Torati ya Mungu wa mbinguni, atalitaka kwenu, na litendeke kwa bidii nyingi,
Kila neno litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke kikamilifu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wa mbinguni. Kwa nini itokee ghadhabu juu ya ufalme wa mfalme na wanawe?
na sehemu ya mafuta iliyoamriwa, katika bathi ya mafuta, itakuwa sehemu ya kumi ya bathi katika kori moja, ambayo ni bathi kumi, yaani homeri; maana bathi kumi ni homeri moja;
Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.