Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Ezra 2:65 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7,337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

tena zaidi ya hao walikuwa na watumwa wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Ezra 2:65
13 Marejeleo ya Msalaba  

Sasa nina miaka themanini; nami je! Naweza kupambanua mema na mabaya? Mimi mtumishi wako, je! Naweza kuonja nilacho au ninywacho? Naweza kusikia tena sauti ya waimbaji wa kiume na wa kike? Kwa nini basi mtumishi wako azidi kumlemea bwana wangu mfalme?


Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.


Basi hilo kusanyiko lote nzima, jumla yake ilikuwa watu elfu arubaini na mbili na mia tatu na sitini,


Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu wao, mia mbili arubaini na watano;


tena zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wanaume kwa wanawake, ambao walikuwa elfu saba na mia tatu na thelathini na saba; kisha walikuwa na waimbaji wanaume kwa wanawake mia mbili arubaini na watano.


Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari.


tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, wanaume kwa wanawake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana.


Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,


Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga watumwa wenzake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;