Kisha itakuwa, mtu huyo nitakayemchagua, fimbo yake itachipuka nami nitayakomesha manung'uniko ya wana wa Israeli, wanung'unikiayo kwangu juu yenu.
Ezra 2:62 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao walitafuta orodha yao katika kumbukumbu za koo, lakini hawakuonekana humo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kushika ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi. Biblia Habari Njema - BHND Hao walitafuta orodha yao katika kumbukumbu za koo, lakini hawakuonekana humo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kushika ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao walitafuta orodha yao katika kumbukumbu za koo, lakini hawakuonekana humo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kushika ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi. Neno: Bibilia Takatifu Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. Neno: Maandiko Matakatifu Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. BIBLIA KISWAHILI Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. |
Kisha itakuwa, mtu huyo nitakayemchagua, fimbo yake itachipuka nami nitayakomesha manung'uniko ya wana wa Israeli, wanung'unikiayo kwangu juu yenu.
Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.
Nawe utawaweka Haruni na wanawe, nao wataushika ukuhani wao, na mgeni atakayekaribia atauawa.