Ezra 2:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Makuhani; wazawa wa Yedaya, wa ukoo wa Yeshua, mia tisa sabini na watatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ifuatayo ni idadi ya makuhani waliorudi kutoka uhamishoni: Makuhani wa ukoo wa Yedaya, waliokuwa wazawa wa Yeshua: 673; Biblia Habari Njema - BHND Ifuatayo ni idadi ya makuhani waliorudi kutoka uhamishoni: Makuhani wa ukoo wa Yedaya, waliokuwa wazawa wa Yeshua: 673; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ifuatayo ni idadi ya makuhani waliorudi kutoka uhamishoni: makuhani wa ukoo wa Yedaya, waliokuwa wazawa wa Yeshua: 673; Neno: Bibilia Takatifu Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua), mia tisa sabini na watatu (973); Neno: Maandiko Matakatifu Makuhani: BIBLIA KISWAHILI Makuhani; wana wa Yedaya, wa ukoo wa Yeshua, mia tisa sabini na watatu. |
Basi, miongoni mwa makuhani walionekana wengine waliokuwa wameoa wanawake wageni; wa wazawa wa wa Yoshua, mwana wa Yosadaki, na nduguze; Maaseya, na Eliezeri, na Yaribu, na Gedalia.
Na wa wazawa wa Pashuri; Elioenai, na Maaseya, na Ishmaeli, na Nethaneli, na Yozabadi, na Elasa.
Ndipo wakasimama Yeshua, na wanawe na ndugu zake, Kadmieli, na wanawe, wana wa Hodavia, pamoja, ili kuwasimamia hao wafanyao kazi katika nyumba ya Mungu; wana wa Henadadi, pamoja na wana wao, na ndugu zao, Walawi.
Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa Torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;