Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Ezra 2:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wa mji wa Betheli na Ai: 223; Biblia Habari Njema - BHND wa mji wa Betheli na Ai: 223; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wa mji wa Betheli na Ai: 223; Neno: Bibilia Takatifu watu wa Betheli na Ai, mia mbili na ishirini na watatu (223); BIBLIA KISWAHILI Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu. |
Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Omboleza, Ee Heshboni, Kwa maana Ai umeangamizwa; Lieni, enyi binti za Raba, Mjivike nguo za magunia; Ombolezeni, mkipiga mbio Huko na huko kati ya maboma; Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa, Makuhani wake na wakuu wake pamoja.
Basi watu wa Betheli walikuwa wamewatuma Shareza na Regem-meleki, na watu wao, ili kuomba fadhili za BWANA,
Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Beth-aveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, Pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai.
Hakusalia mtu yeyote ndani ya Ai, au katika Betheli, asiyetoka nje kuwafuatia Israeli; wakauacha mji wazi na kuwafuatia Israeli.
Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hadi hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.