Na wa wazawa wa Elamu; Matania, na Zekaria, na Yehieli, na Abdi, na Yeremothi, na Eliya.
Ezra 10:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata Shekania, mwana wa Yehieli, mmoja wa wazawa wa Elamu, akajibu, akamwambia Ezra, Sisi tumemkosea Mungu wetu, nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi; lakini bado kuna tumaini kwa Israeli katika jambo hili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo Shekania, mwana wa Yehieli, wa ukoo wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu kwa kuoa wanawake wa kigeni wa nchi hii, lakini hata hivyo bado kuna tumaini kwa ajili ya Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Ndipo Shekania, mwana wa Yehieli, wa ukoo wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu kwa kuoa wanawake wa kigeni wa nchi hii, lakini hata hivyo bado kuna tumaini kwa ajili ya Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo Shekania, mwana wa Yehieli, wa ukoo wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu kwa kuoa wanawake wa kigeni wa nchi hii, lakini hata hivyo bado kuna tumaini kwa ajili ya Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni kutoka mataifa yanayotuzunguka. Lakini pamoja na hili, bado liko tumaini kwa ajili ya Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni kutoka mataifa yanayotuzunguka. Lakini pamoja na hili, bado liko tumaini kwa ajili ya Israeli. BIBLIA KISWAHILI Hata Shekania, mwana wa Yehieli, mmoja wa wana wa Elamu, akajibu, akamwambia Ezra, Sisi tumemkosea Mungu wetu, nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi; lakini bado kuna tumaini kwa Israeli katika jambo hili. |
Na wa wazawa wa Elamu; Matania, na Zekaria, na Yehieli, na Abdi, na Yeremothi, na Eliya.
Na mambo hayo yalipotendeka, wakuu wakanikaribia, wakisema, Watu wa Israeli, na makuhani, na Walawi, hawakujitenga na watu wa nchi hizi, na machukizo yao, yaani, ya Wakanaani, na Wahiti, na Waperizi, na Wayebusi, na Waamoni, na Wamoabi, na Wamisri, na Waamori.
Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na viongozi umetangulia katika kosa hili.
Basi, na sisi, je! Tuwasikilize ninyi kutenda neno hili baya, hata kumkosea Mungu wetu kwa kuwaoa wanawake wageni?
Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako.