Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo.
Ezekieli 8:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo nikaangalia, na tazama, palikuwa na kitu kilichofanana na mwanadamu; kuanzia kilichoonekana kama viuno vyake kwenda chini ilikuwa moto; na kuanzia kilichoonekana kama viuno vyake kwenda juu, ilikuwa mfano wa mwangaza, kama rangi ya kaharabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilipotazama, nikaona maono: Kitu kilichofanana na binadamu. Sehemu yake ya chini, iliyoonekana kama ndio kiuno chake, ilikuwa kama moto. Toka kiuno chake kwenda juu alikuwa na mngao kama wa shaba ingaayo. Biblia Habari Njema - BHND Nilipotazama, nikaona maono: Kitu kilichofanana na binadamu. Sehemu yake ya chini, iliyoonekana kama ndio kiuno chake, ilikuwa kama moto. Toka kiuno chake kwenda juu alikuwa na mngao kama wa shaba ingaayo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilipotazama, nikaona maono: Kitu kilichofanana na binadamu. Sehemu yake ya chini, iliyoonekana kama ndio kiuno chake, ilikuwa kama moto. Toka kiuno chake kwenda juu alikuwa na mng'ao kama wa shaba ing'aayo. Neno: Bibilia Takatifu Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kiuno kuelekea juu sura yake iling’aa vile chuma king’aavyo kikiwa ndani ya moto. Neno: Maandiko Matakatifu Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kwenye kiuno kuelekea juu sura yake kama chuma king’aavyo kikiwa ndani ya moto. BIBLIA KISWAHILI Ndipo nikaangalia, na tazama, palikuwa na kitu kilichofanana na mwanadamu; kuanzia kilichoonekana kama viuno vyake kwenda chini ilikuwa moto; na kuanzia kilichoonekana kama viuno vyake kwenda juu, ilikuwa mfano wa mwangaza, kama rangi ya kaharabu. |
Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo.
Akanileta huko, na tazama, alikuwapo mtu, ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba, naye alikuwa na uzi wa kitani mkononi mwake, na mwanzi wa kupimia; akasimama karibu na lango.
Ikawa katika mwaka wa sita, mwezi wa sita, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa nikikaa nyumbani mwangu, wazee wa Yuda nao wakiwa wamekaa mbele yangu, mkono wa Bwana MUNGU ukaniangukia huko.
mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.