Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA.
Ezekieli 8:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akaniambia tena, Utaona tena machukizo makubwa mengine wanayoyatenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena akaniambia, “Bado utaona machukizo makubwa zaidi wanayotenda.” Biblia Habari Njema - BHND Tena akaniambia, “Bado utaona machukizo makubwa zaidi wanayotenda.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena akaniambia, “Bado utaona machukizo makubwa zaidi wanayotenda.” Neno: Bibilia Takatifu Akasema tena, “Utawaona wakifanya mambo yaliyo chukizo zaidi.” Neno: Maandiko Matakatifu Akasema tena, “Bado utaona machukizo wanayofanya ambayo ni makubwa kuliko haya.” BIBLIA KISWAHILI Akaniambia tena, Utaona tena machukizo makubwa mengine wanayoyatenda. |
Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA.
Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii.
Ndipo akanileta mpaka maingilio ya lango la kaskazini mwa nyumba ya BWANA, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.
Akaniambia, Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, ili niende zangu mbali na patakatifu pangu? Lakini utaona tena machukizo makubwa mengine.
Lakini watu waovu na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.