Tumesikia habari zake; mikono yetu inalegea; dhiki imetushika, na uchungu kama wa mwanamke wakati wa kuzaa kwake.
Ezekieli 7:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mikono yote itakuwa dhaifu, na magoti yote yatalegea kama maji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila mtu, mikono yake itakuwa dhaifu na magoti yake yatakuwa maji. Biblia Habari Njema - BHND Kila mtu, mikono yake itakuwa dhaifu na magoti yake yatakuwa maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila mtu, mikono yake itakuwa dhaifu na magoti yake yatakuwa maji. Neno: Bibilia Takatifu Kila mkono utalegea na kila goti litakuwa dhaifu kama maji. Neno: Maandiko Matakatifu Kila mkono utalegea na kila goti litakuwa dhaifu kama maji. BIBLIA KISWAHILI Mikono yote itakuwa dhaifu, na magoti yote yatalegea kama maji. |
Tumesikia habari zake; mikono yetu inalegea; dhiki imetushika, na uchungu kama wa mwanamke wakati wa kuzaa kwake.
Piga kelele, utoe sauti ya uchungu, Ee mwanadamu, kwa maana upanga u juu ya watu wangu, u juu ya wakuu wote wa Israeli; wametolewa wauawe na upanga pamoja na watu wangu, basi, jipige pajani.
Na itakuwa, wakuambiapo, Mbona unapiga kite? Ndipo utakaposema, Kwa sababu ya habari hizo, maana linakuja; na kila moyo utayeyuka, na mikono yote itakuwa dhaifu, na kila roho itazimia, na magoti yote yatageuka kuwa kama maji; tazama, linakuja, nalo litatendeka, asema Bwana MUNGU.
Je! Moyo wako waweza kuvumilia, au mkono wako waweza kuwa hodari, katika siku zile nitakapokutenda mambo? Mimi, BWANA, nimenena neno hili, tena nitalitenda.
Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.