Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
Ezekieli 5:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC hapo nitakapoiachilia mishale mibaya ya njaa juu yao, mishale iletayo uharibifu nitakayoiachilia ili kuwaharibu ninyi; nami nitaiongeza njaa juu yenu, na tegemeo lenu la mkate nitalivunja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo nitaiachilia mishale yangu mikali ya njaa iwachome na kuangamiza wakazi wako. Nitawafanya wafe njaa kwa kuiharibu akiba yao ya chakula. Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo nitaiachilia mishale yangu mikali ya njaa iwachome na kuangamiza wakazi wako. Nitawafanya wafe njaa kwa kuiharibu akiba yao ya chakula. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo nitaiachilia mishale yangu mikali ya njaa iwachome na kuangamiza wakazi wako. Nitawafanya wafe njaa kwa kuiharibu akiba yao ya chakula. Neno: Bibilia Takatifu Nitakapokurushia mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitairusha ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako. Neno: Maandiko Matakatifu Nitakapokupiga kwa mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitaipiga ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako. BIBLIA KISWAHILI hapo nitakapoiachilia mishale mibaya ya njaa juu yao, mishale iletayo uharibifu nitakayoiachilia ili kuwaharibu ninyi; nami nitaiongeza njaa juu yenu, na tegemeo lenu la mkate nitalivunja. |
Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
Kwa maana, tazama, Bwana, BWANA wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji;
Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwezi, njaa ilizidi sana ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.
Mwanadamu, nchi itakapofanya dhambi na kuniasi, kwa kukosa, nikaunyosha mkono wangu juu yake, na kulivunja tegemeo la chakula chake, na kuiletea njaa, na kukatilia mbali mwanadamu na mnyama;
Tena akaniambia, Mwanadamu, tazama, nitalivunja tegemeo la chakula katika Yerusalemu; nao watakula mkate kwa kuupima, na kwa kuutunza sana; nao watakunywa maji kwa kuyapima, na kwa hofu;
Nayo itakuwa tukano na aibu, na mafundisho na ajabu, kwa mataifa wakuzungukao, hapo nitakapotekeleza hukumu ndani yako, kwa hasira, na kwa ghadhabu, na kwa adhabu kali; mimi, BWANA, nimeyanena hayo;
Nami nitatuma njaa na wanyama wabaya juu yenu, nao watakunyang'anya watu wako; na tauni na damu zitapita ndani yako; nami nitauleta upanga juu yako; mimi BWANA, nimeyanena hayo.
Hapo nitakapovunja tegemeo lenu la mkate, wanawake kumi wataoka mikate yenu katika tanuri moja, nao watawapa mikate yenu tena kwa kupima kwa mizani; nanyi mtakula, lakini hamtashiba.