Nanyi mtaiandika milki ya mji, upana wake elfu tano, na urefu wake elfu ishirini na tano, kandokando ya mahali palipotolewa, iwe sehemu takatifu; nayo itakuwa ya nyumba yote ya Israeli.
Ezekieli 48:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na hao wafanyao kazi mjini, wa kabila zote za Israeli, watailima nchi hiyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafanyakazi wa mjini wa kabila lolote la Israeli wanaweza kulima katika eneo hilo. Biblia Habari Njema - BHND Wafanyakazi wa mjini wa kabila lolote la Israeli wanaweza kulima katika eneo hilo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafanyakazi wa mjini wa kabila lolote la Israeli wanaweza kulima katika eneo hilo. Neno: Bibilia Takatifu Watumishi wa mji wanaolima shamba hili watatoka katika makabila yote ya Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Watumishi wa mji wanaolima shamba hili watatoka katika makabila yote ya Israeli. BIBLIA KISWAHILI Na hao wafanyao kazi mjini, wa kabila zote za Israeli, watailima nchi hiyo. |
Nanyi mtaiandika milki ya mji, upana wake elfu tano, na urefu wake elfu ishirini na tano, kandokando ya mahali palipotolewa, iwe sehemu takatifu; nayo itakuwa ya nyumba yote ya Israeli.
Na mabaki ya urefu wake yaelekeayo matoleo matakatifu, upande wa mashariki yatakuwa mianzi elfu kumi, na upande wa magharibi mianzi elfu kumi; nayo yatakuwa sawasawa na matoleo matakatifu; na mazao yake yatakuwa ni chakula cha watu wafanyao kazi humo mjini.
Matoleo yote yatakuwa mianzi elfu ishirini na tano, kwa mianzi elfu ishirini na tano; mtatoa matoleo matakatifu, nchi ya mraba, pamoja na milki ya mji.