Ezekieli 44:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wala hawatakaribia maiti na kujitia unajisi; ila kwa ajili ya baba, au mama, au mtoto wa kiume, au wa kike, au ndugu mwanamume, au ndugu mwanamke asiyeolewa bado, waweza kujitia unajisi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hawatakaribia maiti ili wasijitie unajisi. Lakini wataweza kujitia unajisi kwa kumkaribia baba au mama au mtoto wa kike au wa kiume au dada yao asiyeolewa, aliyekufa. Biblia Habari Njema - BHND Hawatakaribia maiti ili wasijitie unajisi. Lakini wataweza kujitia unajisi kwa kumkaribia baba au mama au mtoto wa kike au wa kiume au dada yao asiyeolewa, aliyekufa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hawatakaribia maiti ili wasijitie unajisi. Lakini wataweza kujitia unajisi kwa kumkaribia baba au mama au mtoto wa kike au wa kiume au dada yao asiyeolewa, aliyekufa. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Kuhani asijitie unajisi kwa kukaribia maiti; lakini, ikiwa mtu aliyekufa alikuwa baba yake au mama yake, mwana au binti yake, ndugu yake au dada ambaye hakuolewa, basi anaweza kujitia unajisi kwa hao. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Kuhani asijitie unajisi kwa kukaribia maiti, lakini, kama mtu aliyekufa alikuwa baba yake au mama yake, mwana au binti yake, ndugu yake au dada ambaye hajaolewa, basi aweza kujitia unajisi kwa hao. BIBLIA KISWAHILI Wala hawatakaribia maiti na kujitia unajisi; ila kwa ajili ya baba, au mama, au mtoto wa kiume, au wa kike, au ndugu mwanamume, au ndugu mwanamke asiyeolewa bado, waweza kujitia unajisi. |
Mtu yeyote wa kizazi cha Haruni aliye na ukoma, au kisonono; asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu yeyote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka;
Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.