Na milango ya vile vyumba vya mbavuni iliielekea nafasi ile iliyobaki, mlango mmoja ulielekea upande wa kaskazini, na mlango mmoja upande wa kusini; na upana wa nafasi iliyobaki ulikuwa dhiraa tano pande zote.
Ezekieli 41:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Unene wa ukuta uliokuwa wa vile vyumba vya mbavuni, upande wa nje, ulikuwa dhiraa tano; nayo nafasi iliyobaki ilikuwa dhiraa tano; na kati ya vyumba vya mbavuni vya nyumba, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Unene wa ukuta wa nje wa vyumba vya ndani ulikuwa mita mbili u nusu. Nafasi wazi kati ya vyumba vya pembeni mkabala na hekalu Biblia Habari Njema - BHND Unene wa ukuta wa nje wa vyumba vya ndani ulikuwa mita mbili u nusu. Nafasi wazi kati ya vyumba vya pembeni mkabala na hekalu Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Unene wa ukuta wa nje wa vyumba vya ndani ulikuwa mita mbili u nusu. Nafasi wazi kati ya vyumba vya pembeni mkabala na hekalu Neno: Bibilia Takatifu Ukuta wa nje wa vyumba vya pembeni ulikuwa na unene wa dhiraa tano. Eneo la wazi katikati ya vyumba vya pembeni vya Hekalu Neno: Maandiko Matakatifu Ukuta wa nje wa vyumba vya pembeni ulikuwa na unene wa dhiraa tano. Eneo la wazi katikati ya vyumba vya pembeni vya Hekalu BIBLIA KISWAHILI Unene wa ukuta uliokuwa wa vile vyumba vya mbavuni, upande wa nje, ulikuwa dhiraa tano; nayo nafasi iliyobaki ilikuwa dhiraa tano; na kati ya vyumba vya mbavuni vya nyumba, |
Na milango ya vile vyumba vya mbavuni iliielekea nafasi ile iliyobaki, mlango mmoja ulielekea upande wa kaskazini, na mlango mmoja upande wa kusini; na upana wa nafasi iliyobaki ulikuwa dhiraa tano pande zote.
Kisha akaupima ukuta wa nyumba, dhiraa sita; na upana wa kila chumba cha mbavuni, dhiraa nne, kuizunguka nyumba pande zote.
Ndipo akanileta mpaka ua wa nje, njia ya kuelekea upande wa kaskazini; akaniingiza katika chumba kilichopakabili mahali palipotengeka, na kilicholikabili jengo upande wa kaskazini;
Na mbele ya vile vyumba palikuwa na njia, upana wake dhiraa kumi upande wa ndani, njia ya dhiraa mia moja, na milango yake ilielekea upande wa kaskazini.