Na, tazama, kulikuwa na ukuta nje ya nyumba pande zote, na katika mkono wa mtu yule mwanzi wa kupimia, urefu wake dhiraa sita, kila dhiraa, dhiraa na shubiri; basi akaupima upana wa jengo lile, mwanzi mmoja, na urefu wake, mwanzi mmoja.
Ezekieli 41:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena, nikaona ya kwamba nyumba ile ilikuwa na sakafu ya mawe, iliyoinuliwa pande zote; nayo misingi ya vyumba vya mbavuni ilikuwa mwanzi mzima wa dhiraa sita. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, nikaona kuwa hekalu lilikuwa na sakafu iliyonyanyuliwa kulizunguka, nayo ilikuwa ndio msingi wa zile ghorofa tatu mkabala na hekalu, kimo cha msingi wa ghorofa hizo ulikuwa sawa na ule ufito wa kupimia, mita tatu. Biblia Habari Njema - BHND Kisha, nikaona kuwa hekalu lilikuwa na sakafu iliyonyanyuliwa kulizunguka, nayo ilikuwa ndio msingi wa zile ghorofa tatu mkabala na hekalu, kimo cha msingi wa ghorofa hizo ulikuwa sawa na ule ufito wa kupimia, mita tatu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, nikaona kuwa hekalu lilikuwa na sakafu iliyonyanyuliwa kulizunguka, nayo ilikuwa ndio msingi wa zile ghorofa tatu mkabala na hekalu, kimo cha msingi wa ghorofa hizo ulikuwa sawa na ule ufito wa kupimia, mita tatu. Neno: Bibilia Takatifu Nikaona kwamba Hekalu lilikuwa na kitako kilichoinuliwa pande zote; huu ukawa msingi wa vile vyumba vya pembeni. Ulikuwa na urefu wa ule ufito mmoja wa kupimia, yaani dhiraa ndefu sita. Neno: Maandiko Matakatifu Nikaona pia kuwa Hekalu lilikuwa na kitako kilichoinuliwa pande zote, huu ulikuwa ndio msingi wa vile vyumba vya pembeni ambao ulikuwa na urefu wa ule ufito mmoja wa kupimia, yaani, dhiraa ndefu sita. BIBLIA KISWAHILI Tena, nikaona ya kwamba nyumba ile ilikuwa na sakafu ya mawe, iliyoinuliwa pande zote; nayo misingi ya vyumba vya mbavuni ilikuwa mwanzi mzima wa dhiraa sita. |
Na, tazama, kulikuwa na ukuta nje ya nyumba pande zote, na katika mkono wa mtu yule mwanzi wa kupimia, urefu wake dhiraa sita, kila dhiraa, dhiraa na shubiri; basi akaupima upana wa jengo lile, mwanzi mmoja, na urefu wake, mwanzi mmoja.
Na vipimo vya madhabahu kwa dhiraa ni hivi; (dhiraa ni dhiraa na shubiri); kitako chake ni dhiraa moja, na upana wake dhiraa moja; na pambizo yake karibu na ncha yake pande zote, shubiri moja; na hiki kitakuwa kitako cha madhabahu.
Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake ni sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu moja na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.