Ezekieli 41:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na milango hiyo, kila mmoja ulikuwa na mbao mbili; mbao mbili zigeukazo; mbao mbili za mlango mmoja, na mbao mbili za mlango wa pili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Milango hiyo ilikuwa ya tarabe, kwa hiyo kila mlango uliweza kufunguka katikati. Biblia Habari Njema - BHND Milango hiyo ilikuwa ya tarabe, kwa hiyo kila mlango uliweza kufunguka katikati. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Milango hiyo ilikuwa ya tarabe, kwa hiyo kila mlango uliweza kufunguka katikati. Neno: Bibilia Takatifu Kila mlango ulikuwa na vipande viwili, vipande viwili vilivyoshikwa na bawaba vyenye kufunguka kwa kila mlango. Neno: Maandiko Matakatifu Kila mlango ulikuwa na vipande viwili, vipande viwili vilivyoshikwa na bawaba vyenye kufunguka kwa kila mlango. BIBLIA KISWAHILI Na milango hiyo, kila mmoja ulikuwa na mbao mbili; mbao mbili zigeukazo; mbao mbili za mlango mmoja, na mbao mbili za mlango wa pili. |
na milango miwili ya mberoshi; mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa za kukunjana, na mbao mbili za mlango wa pili za kukunjana.
na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.
Ndipo akanileta mpaka ukumbi wa nyumba, akapima kila mwimo wa ukumbi, dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; na upana wa lango ulikuwa dhiraa tatu upande huu, na dhiraa tatu upande huu.
Wewe utakapohusuru mji siku nyingi kwa kufanya vita juu yake, upate kuutwaa, usiangamize miti yake kwa kupeleka shoka juu yake, kwani utaweza kula matunda yake; wala usiiteme, kwa maana huo mti wa kondeni, je! Ni mtu, hata ukauzuie?