Ezekieli 41:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na hilo hekalu, miimo ya milango yake ilikuwa ya miraba; na mbele ya patakatifu kuonekana kwake palionekana kama hapo kwanza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Miimo ya mahali patakatifu ilikuwa ya mraba. Mbele ya mlango wa kuingilia mahali patakatifu kabisa kulikuwa na kitu kilichoonekana kama Biblia Habari Njema - BHND Miimo ya mahali patakatifu ilikuwa ya mraba. Mbele ya mlango wa kuingilia mahali patakatifu kabisa kulikuwa na kitu kilichoonekana kama Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Miimo ya mahali patakatifu ilikuwa ya mraba. Mbele ya mlango wa kuingilia mahali patakatifu kabisa kulikuwa na kitu kilichoonekana kama Neno: Bibilia Takatifu Mahali patakatifu pa nje palikuwa na miimo ya mlango uliokuwa mraba; na ule uliokuwa katika Patakatifu Pa Patakatifu ulifanana na huo. Neno: Maandiko Matakatifu Mahali patakatifu pa nje palikuwa na miimo ya mlango uliokuwa mraba na ule uliokuwa katika Patakatifu Pa Patakatifu ulikuwa unafanana na huo mwingine. BIBLIA KISWAHILI Na hilo hekalu, miimo ya milango yake ilikuwa ya miraba; na mbele ya patakatifu kuonekana kwake palionekana kama hapo kwanza. |
Akafanya miimo pia, dhiraa sitini; na uwanda uliufikia mwimo, lango lile likizungukwa pande zote.
Kisha akaupima ukumbi wa lango, dhiraa nane; na miimo yake, dhiraa mbili; na ukumbi wa lango uliielekea nyumba.
Akanileta mpaka hekaluni, akaipima miimo, upana wake dhiraa sita upande mmoja, na upana wake dhiraa sita upande wa pili, ambao ulikuwa ni upana wa maskani.