Ezekieli 41:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na upana wa maingilio yake ulikuwa dhiraa kumi; na mbavu za maingilio zilikuwa dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; akaupima urefu wake, dhiraa arubaini, na upana wake, dhiraa ishirini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na upana wa mita 5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita 2.5. Akaupima ukumbi wenyewe, nao ulikuwa na urefu wa mita 20 na upana mita 10. Biblia Habari Njema - BHND na upana wa mita 5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita 2.5. Akaupima ukumbi wenyewe, nao ulikuwa na urefu wa mita 20 na upana mita 10. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na upana wa mita 5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita 2.5. Akaupima ukumbi wenyewe, nao ulikuwa na urefu wa mita 20 na upana mita 10. Neno: Bibilia Takatifu Ingilio lilikuwa la upana wa dhiraa kumi, na kuta zilizochomoza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa tano. Pia akapima ukumbi mkuu; ulikuwa na urefu wa dhiraa arobaini, na upana wa dhiraa ishirini. Neno: Maandiko Matakatifu Ingilio lilikuwa la upana wa dhiraa kumi na kuta zilizojitokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa tano. Pia akapima sehemu ya nje ya patakatifu, nayo ilikuwa na urefu wa dhiraa arobaini na upana wa dhiraa ishirini. BIBLIA KISWAHILI Na upana wa maingilio yake ulikuwa dhiraa kumi; na mbavu za maingilio zilikuwa dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; akaupima urefu wake, dhiraa arobaini, na upana wake, dhiraa ishirini. |
Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea BWANA, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini.
Tena wameifunga milango ya ukumbi, na kuzizima taa, wala hawakufukiza uvumba, wala hawakumtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa katika patakatifu.
Basi hivi ndivyo vipimo vya majengo ya nyumba ya Mungu alivyoviweka Sulemani. Urefu wake ulikuwa dhiraa sitini na upana wake dhiraa ishirini.
Tena, akaifunikiza kwa dhahabu nyumba, na boriti, na vizingiti, na kuta zake, na milango yake; akachora makerubi kutani.
Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa Hema, cha nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji wa taraza.
Kisha akafanya pazia la sitara kwa ajili ya mlango wa Hema, la nguo ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa, kazi ya mwenye kutia taraza,
Baadaye akanileta tena mpaka lango la nyumba; na tazama, maji yalitoka chini ya kizingiti cha nyumba, kwa njia ya mashariki, maana upande wa mbele wa nyumba ulielekea upande wa mashariki; nayo maji yakashuka toka chini ya upande wa kulia wa nyumba, upande wa kusini wa madhabahu.
Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.