Ezekieli 39:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo, watu waishio katika miji ya Israeli watatoka na kukusanya silaha zilizoachwa na kuzichoma moto. Watatumia hizo ngao, pinde, mishale, mikuki na marungu, kama kuni za kuwasha moto kwa muda wa miaka saba. Biblia Habari Njema - BHND Hapo, watu waishio katika miji ya Israeli watatoka na kukusanya silaha zilizoachwa na kuzichoma moto. Watatumia hizo ngao, pinde, mishale, mikuki na marungu, kama kuni za kuwasha moto kwa muda wa miaka saba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo, watu waishio katika miji ya Israeli watatoka na kukusanya silaha zilizoachwa na kuzichoma moto. Watatumia hizo ngao, pinde, mishale, mikuki na marungu, kama kuni za kuwasha moto kwa muda wa miaka saba. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani, kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni. BIBLIA KISWAHILI Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba; |
Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
hata hawataokota kuni mashambani, wala hawatakata kuni msituni; maana watafanya mioto kwa silaha zile; nao watawateka nyara watu waliowateka wao, na kuwapora watu waliowapora wao, asema Bwana MUNGU.
Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiria mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
Na macho yenu ninyi yataona, nanyi mtasema, BWANA ndiye mkuu hata katika nje ya mipaka ya Israeli.
BWANA akamwambia Yoshua, Wewe usiogope kwa ajili ya hao; kwani kesho wakati kama huu nitawatoa wakiwa wameuawa wote mbele ya Israeli; utawakata farasi wao, na magari yao utayateketeza kwa moto.