Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na jamii ya watu wake wote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.
Ezekieli 39:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na kwa muda wa miezi saba, nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuitakasa nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa kuisafisha nchi Waisraeli watatumia muda wa miezi saba kuzika maiti hizo. Biblia Habari Njema - BHND Kwa kuisafisha nchi Waisraeli watatumia muda wa miezi saba kuzika maiti hizo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa kuisafisha nchi Waisraeli watatumia muda wa miezi saba kuzika maiti hizo. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Kwa miezi saba nyumba ya Israeli itakuwa ikiwazika ili kuisafisha nchi. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Kwa miezi saba nyumba ya Israeli itakuwa ikiwazika ili kuisafisha nchi. BIBLIA KISWAHILI Na kwa muda wa miezi saba, nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuitakasa nchi. |
Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na jamii ya watu wake wote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.
Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watachunguza.
Hii ndiyo amri, mtu afapo ndani ya hema; kila mtu aingiaye ndani ya hema hiyo, na kila mtu aliye humo hemani, atakuwa najisi muda wa siku saba.
Kisha mtu yeyote huko nje shambani atakayemgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga, au mfupa wa mtu, au kaburi, atakuwa najisi muda wa siku saba.
mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi wako.