Ole wangu mimi! Kwa kuwa ni mgeni katika Mesheki; Na kufanya makao yangu Katikati ya hema za Kedari.
Ezekieli 39:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wewe, mwanadamu, tabiri juu ya Gogu, useme, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bwana Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu! Toa unabii dhidi ya Gogu. Mwambie, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi nitapambana nawe Gogu mtawala mkuu wa mataifa ya Mesheki na Tubali. Biblia Habari Njema - BHND Bwana Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu! Toa unabii dhidi ya Gogu. Mwambie, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi nitapambana nawe Gogu mtawala mkuu wa mataifa ya Mesheki na Tubali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bwana Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu! Toa unabii dhidi ya Gogu. Mwambie, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi nitapambana nawe Gogu mtawala mkuu wa mataifa ya Mesheki na Tubali. Neno: Bibilia Takatifu “Mwanadamu, tabiri dhidi ya Gogu useme: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ee Gogu mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali. Neno: Maandiko Matakatifu “Mwanadamu, tabiri dhidi ya Gogu useme: ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Ee Gogu mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali. BIBLIA KISWAHILI Na wewe, mwanadamu, tabiri juu ya Gogu, useme, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali; |
Ole wangu mimi! Kwa kuwa ni mgeni katika Mesheki; Na kufanya makao yangu Katikati ya hema za Kedari.
Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia;
Ugiriki na Tubali na Mesheki ndio waliokuwa wachuuzi wako; walitoa wanadamu, na vyombo vya shaba, kwa biashara yako.
Mesheki yuko huko, na Tubali, na watu wake umati wote; makaburi yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana walitisha katika nchi ya walio hai.
uuambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima Seiri, nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, nami nitakufanya kuwa ukiwa na ajabu.
nami nitakugeuza na kukuongoza, nami nitakupandisha toka pande za mwisho za kaskazini; nami nitakuleta juu ya milima ya Israeli;
Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi; nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nitawalalisha salama salimini.
Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.
Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitayainua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.
naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.