Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Na kivuli wakati wa joto; Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa, Kama dhoruba ipigayo ukuta.
Ezekieli 38:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utakwenda kasi kama tufani na kuifunika nchi kama wingu, wewe mwenyewe na jeshi lako lote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe. Biblia Habari Njema - BHND Utakwenda kasi kama tufani na kuifunika nchi kama wingu, wewe mwenyewe na jeshi lako lote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utakwenda kasi kama tufani na kuifunika nchi kama wingu, wewe mwenyewe na jeshi lako lote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe. Neno: Bibilia Takatifu Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu. Neno: Maandiko Matakatifu Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu. BIBLIA KISWAHILI Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe. |
Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Na kivuli wakati wa joto; Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa, Kama dhoruba ipigayo ukuta.
Tazama, Bwana ana mmoja aliye hodari, mwenye nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe, tufani iharibuyo, kama dhoruba ya maji mengi yafurikayo, ndivyo atakavyotupa chini kwa mkono.
Mishale yao ni mikali, na pinde zao zote zimepindika; Kwato za farasi wao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli;
Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi wake ni wepesi kuliko tai. Ole wetu, kwa sababu tumeharibika.
basi waambie hao wanaoupaka ukuta chokaa isiyokorogwa vema, ya kwamba utaanguka; kutakuwa mvua ya kufurika; nanyi, enyi mvua ya mawe makubwa ya barafu, mtaanguka; na upepo wa dhoruba utaupasua.
Huko Tapanesi nako mchana utakuwa giza, nitakapovunja huko kongwa za Misri, na kiburi cha uwezo wake kitakoma ndani yake, na katika habari zake, wingu litaifunika, na binti zake watakwenda utumwani.
nawe utapanda juu uwajie watu wangu, Israeli, kama wingu likiifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kupitia kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.
Na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati.
siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.
Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.