Ezekieli 38:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wewe Gogu! Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ile itakapofika utaanza kuwaza moyoni mwako na kupanga mipango miovu na kusema: Biblia Habari Njema - BHND “Wewe Gogu! Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ile itakapofika utaanza kuwaza moyoni mwako na kupanga mipango miovu na kusema: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Wewe Gogu! Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ile itakapofika utaanza kuwaza moyoni mwako na kupanga mipango miovu na kusema: Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya. BIBLIA KISWAHILI Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya; |
Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache.
Roho ya BWANA ikaniangukia, naye akaniambia, Nena, BWANA asema hivi; Mmesema maneno hayo, Enyi nyumba ya Israeli; maana mimi nayajua yaingiayo katika mioyo yenu.
Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.
Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, moyo wa kumsaliti;
Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuhifadhi kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.
Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili ikiwezekana, usamehewe fikira hii ya moyo wako.
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.