Mwanadamu, nyumba ya Israeli, je! Nyumba ile iliyoasi, hawakukuambia, Unafanya nini wewe?
Ezekieli 37:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wana wa watu wangu watakapokuambia, wakisema, Je! Hutatuonesha maana ya mambo hayo utendayo? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wananchi wenzako watakapouliza, ‘Je, hutatueleza maana ya jambo hilo?’ Biblia Habari Njema - BHND Wananchi wenzako watakapouliza, ‘Je, hutatueleza maana ya jambo hilo?’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wananchi wenzako watakapouliza, ‘Je, hutatueleza maana ya jambo hilo?’ Neno: Bibilia Takatifu “Watu wako watakapokuuliza, ‘Je, hutatuambia ni nini maana ya jambo hili?’ Neno: Maandiko Matakatifu “Watu wako watakapokuuliza, ‘Je, hutatuambia ni nini maana ya jambo hili?’ BIBLIA KISWAHILI Na wana wa watu wangu watakapokuambia, wakisema, Je! Hutatuonesha maana ya mambo hayo utendayo? |
Mwanadamu, nyumba ya Israeli, je! Nyumba ile iliyoasi, hawakukuambia, Unafanya nini wewe?
Waambie sasa nyumba hii iliyoasi, Hamjui maana ya mambo haya? Waambie, Tazama, mfalme wa Babeli alifika Yerusalemu, akamtwaa mfalme wake, na wakuu wake, akawachukua pamoja naye mpaka Babeli;
Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, wao hunisema; Je! Mtu huyu si mtu mwenye kupiga mithali?
Watu hao wakaniambia, Je! Hutaki kutuambia maana ya mambo haya kwetu, hata umefanya kama vile ufanyavyo.
Mwanadamu, sema na wana wa watu wako, uwaambie, Hapo nitakapoleta upanga juu ya nchi, watu wa nchi hiyo wakimtwaa mtu mmoja miongoni mwao, na kumweka awe mlinzi wao;
Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na makabila ya Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja mkononi mwangu.