Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu.
Ezekieli 37:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti kimoja, viwe kimoja katika mkono wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Halafu vichukue vijiti hivyo na kuvishikamanisha ili vionekane kama kijiti kimoja. Biblia Habari Njema - BHND Halafu vichukue vijiti hivyo na kuvishikamanisha ili vionekane kama kijiti kimoja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Halafu vichukue vijiti hivyo na kuvishikamanisha ili vionekane kama kijiti kimoja. Neno: Bibilia Takatifu Ziunganishe pamoja kuwa fimbo moja ili ziwe fimbo moja katika mkono wako. Neno: Maandiko Matakatifu Ziunganishe pamoja kuwa fimbo moja ili kwamba ziwe fimbo moja katika mkono wako. BIBLIA KISWAHILI ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti kimoja, viwe kimoja katika mkono wako. |
Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu.
Katika siku hizo, na wakati huo, asema BWANA, wana wa Israeli watakuja, wao na wana wa Yuda pamoja; Wataendelea njiani mwao wakilia, nao watamtafuta BWANA, Mungu wao.
Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajichagulia kiongozi mmoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.
Maana hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliitia jina la BWANA, wamtumikie kwa nia moja.