Ezekieli 36:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC basi katika kutabiri habari za nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nimenena katika wivu wangu na hasira yangu, kwa sababu mmetukanwa na mataifa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii kuhusu nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema mambo haya kutokana na ghadhabu yangu yenye wivu juu ya nchi yangu, kwa sababu imetukanwa na watu wa mataifa. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii kuhusu nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema mambo haya kutokana na ghadhabu yangu yenye wivu juu ya nchi yangu, kwa sababu imetukanwa na watu wa mataifa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii kuhusu nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema mambo haya kutokana na ghadhabu yangu yenye wivu juu ya nchi yangu, kwa sababu imetukanwa na watu wa mataifa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa. BIBLIA KISWAHILI basi katika kutabiri habari za nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nimenena katika wivu wangu na hasira yangu, kwa sababu mmetukanwa na mataifa; |
Nami nitawainulia miche iwe sifa njema, wala hawataangamizwa kwa njaa katika nchi yao tena, wala hawatatukanwa tena na mataifa.
wala sitakuacha usikie matusi ya wasioamini, wala hutaaibishwa na watu tena; wala hutalikwaza taifa lako tena, asema Bwana MUNGU.
basi Bwana MUNGU asema hivi; Nimeinua mkono wangu, kusema, Hakika, mataifa walio karibu nanyi pande zote, nao watatukanwa.
Itakuwa katika siku hiyo, Gogu atakapokuja kupigana na nchi ya Israeli, asema Bwana MUNGU, ghadhabu yangu itapanda.
Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;
Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao.