Akasema, Niliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji; BWANA akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
Ezekieli 35:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Miji yako nitaiharibu, nawe utakuwa ukiwa; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ninaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa jangwa. Ndipo utakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Ninaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa jangwa. Ndipo utakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ninaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa jangwa. Ndipo utakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi bwana. BIBLIA KISWAHILI Miji yako nitaiharibu, nawe utakuwa ukiwa; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. |
Akasema, Niliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji; BWANA akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Basi wakafanya hivyo.
Kwani wakati huu nitaleta mapigo yangu yote juu ya moyo wako, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako; ili upate kujua ya kuwa hapana mmoja mfano wa mimi ulimwenguni kote.
Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeyasikia matusi yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale.
Kama vile ulivyofurahi juu ya urithi wa nyumba ya Israeli, kwa sababu ilikuwa ukiwa, ndivyo nitakavyokutenda wewe; utakuwa ukiwa, Ee mlima Seiri, na Edomu yote, naam, yote pia; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Nitakufanya kuwa ukiwa wa daima, na miji yako haitakaliwa na watu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.