Ezekieli 33:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo watakapojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoifanya nchi kuwa ukiwa na ajabu, kwa sababu ya machukizo yao yote waliyoyatenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naam, nitakapoifanya hiyo nchi kuwa jangwa na tupu kwa sababu ya mambo yote ya kuchukiza waliyotenda, ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema - BHND Naam, nitakapoifanya hiyo nchi kuwa jangwa na tupu kwa sababu ya mambo yote ya kuchukiza waliyotenda, ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naam, nitakapoifanya hiyo nchi kuwa jangwa na tupu kwa sababu ya mambo yote ya kuchukiza waliyotenda, ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.” Neno: Bibilia Takatifu Kisha watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapokuwa nimeifanya nchi ukiwa kwa sababu ya mambo yote ya machukizo waliyotenda.’ Neno: Maandiko Matakatifu Kisha watajua kuwa Mimi ndimi bwana, nitakapokuwa nimeifanya nchi kuwa ukiwa na utupu kwa sababu ya mambo yote ya machukizo waliyotenda.’ BIBLIA KISWAHILI Ndipo watakapojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoifanya nchi kuwa ukiwa na ajabu, kwa sababu ya machukizo yao yote waliyoyatenda. |
Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi wake.
ili kufanya nchi yao kuwa kitu cha kushangaza, na cha kuzomewa daima; kila mtu apitaye karibu nayo atashangaa, na kutikisa kichwa chake.
Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.
Nao watawalipa ninyi malipo ya uasherati wenu, nanyi mtachukua dhambi za vinyago vyenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa na ajabu, na kiburi cha uwezo wake kitakoma; nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa, asipite mtu.
Nawe, mwanadamu, wana wa watu wako husimulia habari zako karibu na kuta, na ndani ya milango ya nyumba zao, na kuambiana, kila mtu na ndugu yake, wakisema, Haya! Twende tukasikie ni neno gani hilo litokalo kwa BWANA.
Na hayo yatakapokuwapo (tazama, yanakuja), ndipo watakapojua ya kuwa nabii amekuwapo kati yao.
Nami nitakutenda nisiyoyatenda zamani, wala sitafanya tena mambo kama hayo, kwa sababu ya machukizo yako yote.
Bwana MUNGU asema hivi; Piga kwa mkono wako, ipige nchi kwa mguu wako, ukaseme, Ole! Kwa sababu ya machukizo maovu yote ya nyumba ya Israeli; maana wataanguka kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni.
Mfalme ataomboleza, na mkuu atavikwa ukiwa, na mikono ya watu wa nchi itataabika; nitawatenda kulingana na njia yao; nami nitawahukumu kulingana na kustahili kwao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Jicho langu halitakuachilia, wala sitaona huruma; bali nitakupatiliza njia zako, na machukizo yako yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.