Na jeshi lote la Wakaldayo, waliokuwa pamoja na huyo kamanda wa askari walinzi, wakazibomoa kuta za Yerusalemu pande zote.
Ezekieli 33:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikawa, katika mwaka wa kumi na mbili wa kuhamishwa kwetu, mwezi wa kumi, siku ya tano ya mwezi, mtu mmoja aliyekuwa ametoroka toka Yerusalemu akanijia, akisema, Mji umetekwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku ya tano ya mwezi wa kumi, mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mtu mmoja aliyetoroka kutoka Yerusalemu alinijia, akasema: “Mji wa Yerusalemu umetekwa!” Biblia Habari Njema - BHND Siku ya tano ya mwezi wa kumi, mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mtu mmoja aliyetoroka kutoka Yerusalemu alinijia, akasema: “Mji wa Yerusalemu umetekwa!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku ya tano ya mwezi wa kumi, mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mtu mmoja aliyetoroka kutoka Yerusalemu alinijia, akasema: “Mji wa Yerusalemu umetekwa!” Neno: Bibilia Takatifu Mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mwezi wa kumi, siku ya tano, mtu aliyekuwa ametoroka kutoka Yerusalemu akanijia na kusema, “Mji wa Yerusalemu umeanguka!” Neno: Maandiko Matakatifu Mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mwezi wa kumi, siku ya tano, mtu aliyekuwa ametoroka kutoka Yerusalemu akanijia na kusema, “Mji wa Yerusalemu umeanguka!” BIBLIA KISWAHILI Ikawa, katika mwaka wa kumi na mbili wa kuhamishwa kwetu, mwezi wa kumi, siku ya tano ya mwezi, mtu mmoja aliyekuwa ametoroka toka Yerusalemu akanijia, akisema, Mji umetekwa. |
Na jeshi lote la Wakaldayo, waliokuwa pamoja na huyo kamanda wa askari walinzi, wakazibomoa kuta za Yerusalemu pande zote.
Ndipo mahali pakabomolewa katika ukuta wa mji, watu wote wa vita wakakimbia usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wakiuzuia mji pande zote;) mfalme akaenda kwa njia ya Araba.
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua akiwa amefungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa wakiwa wamefungwa mpaka Babeli.
Siku ya tano ya mwezi, nao ulikuwa ni mwaka wa tano wa kuhamishwa kwake mfalme Yehoyakini,
Tena, katika mwaka wa tisa, mwezi wa kumi, siku ya kumi ya mwezi, neno la BWANA likanijia, kusema,
Mwanadamu, liandike jina la siku hii, naam, la siku ii hii; mfalme wa Babeli ameuzingira Yerusalemu siku ii hii.
Ikawa katika mwaka wa kumi na mmoja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA likanijia, kusema,
Ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA likanijia, kusema,
Ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno la BWANA likanijia kusema,
Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu, mwanzo wa mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kupigwa mji, siku iyo hiyo, mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, akanileta huko.