Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.
Ezekieli 32:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Umemshinda nani kwa uzuri? Shuka, ukalazwe pamoja na wasiotahiriwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waambie: Nyinyi ni wazuri kuliko nani? Nendeni kuzimu mlazwe pamoja na wasiomjua Mungu! Biblia Habari Njema - BHND Waambie: Nyinyi ni wazuri kuliko nani? Nendeni kuzimu mlazwe pamoja na wasiomjua Mungu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waambie: Nyinyi ni wazuri kuliko nani? Nendeni kuzimu mlazwe pamoja na wasiomjua Mungu! Neno: Bibilia Takatifu Je, ninyi mmekubalika zaidi ya wengine? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa! Neno: Maandiko Matakatifu Je, ninyi mnamzidi nani kwa uzuri? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa! BIBLIA KISWAHILI Umemshinda nani kwa uzuri? Shuka, ukalazwe pamoja na wasiotahiriwa. |
Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.
Umefanana na nani, hivi katika utukufu na ukuu, kati ya miti ya Adeni? Lakini utashushwa pamoja na miti ya Adeni, hata pande za chini za nchi; utalala kati ya hao wasiotahiriwa; pamoja na hao waliouawa kwa upanga. Huyu ndiye Farao, na jamii yote ya watu wake, asema Bwana MUNGU.
Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri, na jamii ya watu wake, Je! Umefanana na nani katika ukuu wako?
Walio hodari watasema naye, toka kati ya kuzimu pamoja nao wamsaidiao; wameshuka wamelala kimya, hata wasiotahiriwa, wakiwa wameuawa kwa upanga.
Elamu yuko huko, na watu wake umati wote, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka wakiwa hawajatahiriwa hadi pande za chini ya nchi; ambao waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.
Mesheki yuko huko, na Tubali, na watu wake umati wote; makaburi yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana walitisha katika nchi ya walio hai.
Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?
Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.