Tena nitawaangaza mifugo wake wote, toka kando ya maji mengi; na mguu wa mwanadamu hautayatibua tena, wala kwato za mnyama hazitayatibua.
Ezekieli 32:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo nitakapoyafanya maji yao kuwa safi, na kuiendesha mito yao kama mafuta, asema Bwana MUNGU. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo nitayafanya maji yake yatulie na kuitiririsha mito yake kama mafuta. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema - BHND Hapo nitayafanya maji yake yatulie na kuitiririsha mito yake kama mafuta. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo nitayafanya maji yake yatulie na kuitiririsha mito yake kama mafuta. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Neno: Bibilia Takatifu Kisha nitafanya maji yake yatulie na kufanya vijito vyake vitiririke kama mafuta, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha nitafanya maji yake yatulie na kufanya vijito vyake vitiririke kama mafuta, asema bwana Mwenyezi. BIBLIA KISWAHILI Ndipo nitakapoyafanya maji yao kuwa safi, na kuiendesha mito yao kama mafuta, asema Bwana MUNGU. |
Tena nitawaangaza mifugo wake wote, toka kando ya maji mengi; na mguu wa mwanadamu hautayatibua tena, wala kwato za mnyama hazitayatibua.
Nitakapoifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa na jangwa, nchi iliyopungukiwa na vitu vilivyoijaza, nitakapowapiga watu wote wakaao ndani yake, ndipo watakapojua ya kuwa mimi ndimi BWANA.