Hautapita kati yake mguu wa mwanadamu, wala hautapita kati yake mguu wa mnyama, wala haitakaliwa na watu, muda wa miaka arubaini.
Ezekieli 32:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena nitawaangaza mifugo wake wote, toka kando ya maji mengi; na mguu wa mwanadamu hautayatibua tena, wala kwato za mnyama hazitayatibua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitaiangamiza mifugo yako yote kando ya mto Nili. Maji yake hayatavurugwa tena na mtu wala kwato za mnyama kuyachafua tena. Biblia Habari Njema - BHND Nitaiangamiza mifugo yako yote kando ya mto Nili. Maji yake hayatavurugwa tena na mtu wala kwato za mnyama kuyachafua tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitaiangamiza mifugo yako yote kando ya mto Nili. Maji yake hayatavurugwa tena na mtu wala kwato za mnyama kuyachafua tena. Neno: Bibilia Takatifu Nitaangamiza mifugo yake yote wanaojilisha kando ya maji mengi: hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu wala kwato za mnyama hazitayachafua tena. Neno: Maandiko Matakatifu Nitaangamiza mifugo yake yote wanaojilisha kando ya maji mengi, hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu wala kwato za mnyama hazitayachafua tena. BIBLIA KISWAHILI Tena nitawaangamizia mifugo yake yote, toka kando ya maji mengi; na mguu wa mwanadamu hautayatibua tena, wala kwato za mnyama hazitayatibua. |
Hautapita kati yake mguu wa mwanadamu, wala hautapita kati yake mguu wa mnyama, wala haitakaliwa na watu, muda wa miaka arubaini.
Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitaleta upanga juu yako, nami nitakatilia mbali nawe wanadamu na wanyama.
Nami nitaikausha mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi, BWANA, nimenena neno hili.
Ndipo nitakapoyafanya maji yao kuwa safi, na kuiendesha mito yao kama mafuta, asema Bwana MUNGU.
Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwanasimba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.
Je! Mwaona ya kuwa ni neno dogo ninyi kulishwa malisho mema, hata mkawa hamna budi kukanyaga kwa miguu yenu yaliyosalia? Na kuwa mmekunywa maji yaliyo safi, nanyi hamna budi kuyatibua kwa miguu yaliyobaki?