Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atashtuka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini BWANA ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?
Ezekieli 32:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nami nitawashangaza watu wa kabila nyingi kwa habari zako, na wafalme wao wataogopa sana kwa ajili yako, nitakapoutikisa upanga wangu mbele yao; nao watatetemeka kila dakika, kila mtu kwa ajili ya uhai wake, katika siku ya kuanguka kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitayashtusha mataifa mengi kwa habari zako, wafalme wao watatetemeka kwa sababu yako, nitakaponyosha upanga wangu mbele yao. Watatetemeka kila wakati, kila mtu akihofia uhai wake, siku ile ya kuangamia kwako. Biblia Habari Njema - BHND Nitayashtusha mataifa mengi kwa habari zako, wafalme wao watatetemeka kwa sababu yako, nitakaponyosha upanga wangu mbele yao. Watatetemeka kila wakati, kila mtu akihofia uhai wake, siku ile ya kuangamia kwako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitayashtusha mataifa mengi kwa habari zako, wafalme wao watatetemeka kwa sababu yako, nitakaponyosha upanga wangu mbele yao. Watatetemeka kila wakati, kila mtu akihofia uhai wake, siku ile ya kuangamia kwako. Neno: Bibilia Takatifu Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie, wafalme wao watatetemeka kwa hofu kwa ajili yako nitakapotikisa upanga wangu mbele yao. Siku ya anguko lako kila mmoja wao atatetemeka kila dakika kwa ajili ya maisha yake. Neno: Maandiko Matakatifu Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie, wafalme wao watatetemeka kwa hofu kwa ajili yako nitakapotikisa upanga wangu mbele yao. Siku ya anguko lako kila mmoja wao atatetemeka kila dakika kwa ajili ya maisha yake. BIBLIA KISWAHILI Nami nitawashangaza watu wa kabila nyingi kwa habari zako, na wafalme wao wataogopa sana kwa ajili yako, nitakapoutikisa upanga wangu mbele yao; nao watatetemeka kila dakika, kila mtu kwa ajili ya uhai wake, katika siku ya kuanguka kwako. |
Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atashtuka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini BWANA ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?
Na kila pigo la fimbo iliyoamriwa, ambayo BWANA ataliweka juu yake, litakuwa pamoja na matari na vinanda, na kwa mapigano yenye kutikisa atapigana nao.
Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.
Ndipo wakuu wote wa bahari watashuka kutoka viti vyao vya enzi, na kuweka upande mavazi yao, na kuvua nguo zao zilizotiwa taraza; watajivika wakitetemeka; wataketi na kutetemeka kila dakika, na kukustaajabia,
Wote wakaao katika visiwa vile watakustaajabia, na wafalme wao wameogopa sana, wamefadhaika nyuso zao.
Katika siku hiyo watatoka wajumbe mbele zangu katika merikebu, ili kuwatia hofu Wakushi, wanaojiona kuwa salama, na dhiki itakuwa juu yao, vile vile kama katika siku ya Misri; kwa maana, tazama, inakuja.
Piga yowe, msonobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.
mataifa yote watasema, Mbona BWANA ameifanyia hivi nchi hii? Ni nini maana yake joto la hasira hizi kubwa?
Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia.
wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.