Ezekieli 31:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndege wote wa angani walifanya viota vyao katika vitanzu vyake, na chini ya matawi yake wanyama wote wa kondeni walizaa watoto wao, na chini ya uvuli wake mataifa makuu yote walikaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndege wote waliweka viota matawini mwake, chini yake wanyama walizaliwa, mataifa yote makubwa yaliburudika kivulini mwake. Biblia Habari Njema - BHND Ndege wote waliweka viota matawini mwake, chini yake wanyama walizaliwa, mataifa yote makubwa yaliburudika kivulini mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndege wote waliweka viota matawini mwake, chini yake wanyama walizaliwa, mataifa yote makubwa yaliburudika kivulini mwake. Neno: Bibilia Takatifu Ndege wote wa angani wakaweka viota kwenye vitawi vyake, wanyama wote wa shambani wakazaana chini ya matawi yake, mataifa makubwa yote yaliishi chini ya kivuli chake. Neno: Maandiko Matakatifu Ndege wote wa angani wakaweka viota kwenye vitawi vyake, wanyama wote wa shambani wakazaana chini ya matawi yake, mataifa makubwa yote yaliishi chini ya kivuli chake. BIBLIA KISWAHILI Ndege wote wa angani walifanya viota vyao katika vitanzu vyake, na chini ya matawi yake wanyama wote wa kondeni walizaa watoto wao, na chini ya uvuli wake mataifa makuu yote walikaa. |
juu ya mlima wa mahali palipoinuka pa Israeli nitakipanda; nacho kitatoa matawi, na kuzaa matunda, nao utakuwa mwerezi mzuri; na chini yake watakaa ndege wa kila namna ya mbawa; katika uvuli wa matawi yake watakaa.
Juu ya magofu yake ndege wote wa angani watakaa, na wanyama wote wa jangwani watakuwa juu ya matawi yake;
Hao nao waliteremka kuzimuni pamoja naye kwa watu waliouawa kwa upanga; naam, wale waliowasaidia, waliokaa chini ya uvuli wake kati ya mataifa.
Basi hivyo alikuwa mzuri katika ukuu wake, katika urefu wa matawi yake; maana mizizi yake ilikuwa karibu na maji mengi.
Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; niliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana.
Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa mwituni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.
ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote; ambao chini yake wanyama wa mwituni walikaa, na ndege wa angani walikuwa na makao yao katika matawi yake;
nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko miboga yote ikawa mti, hata ndege wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake.