Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Ezekieli 31:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Bwana MUNGU asema hivi, Katika siku ile alipoteremka mpaka kuzimu niliamuru matanga, nilikifunika kilindi kwa ajili yake, nikiizuia mito yake, nayo maji makuu yalizuiwa; niliamuru Lebanoni kumwombolezea, na miti yote ya shambani ilizimia kwa ajili yake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ileile mwerezi ulipofika kuzimu nilitandaza giza nene juu yake nikaufunika; mito yake niliikausha na mtiririko wa maji yake mengi nikaukomesha. Nayo Lebanoni niliiweka gizani kwa ajili yake, na miti yote msituni ikazirai kwa ajili yake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku ileile mwerezi ulipofika kuzimu nilitandaza giza nene juu yake nikaufunika; mito yake niliikausha na mtiririko wa maji yake mengi nikaukomesha. Nayo Lebanoni niliiweka gizani kwa ajili yake, na miti yote msituni ikazirai kwa ajili yake.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Bwana MUNGU asema hivi, Katika siku ile alipoteremka mpaka kuzimu niliamuru matanga, nilikifunika kilindi kwa ajili yake, nikiizuia mito yake, nayo maji makuu yalizuiwa; niliamuru Lebanoni kumwombolezea, na miti yote ya shambani ilizimia kwa ajili yake.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Ezekieli 31:15
8 Marejeleo ya Msalaba  

Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo; Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa, Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.

Ndipo wakuu wote wa bahari watashuka kutoka viti vyao vya enzi, na kuweka upande mavazi yao, na kuvua nguo zao zilizotiwa taraza; watajivika wakitetemeka; wataketi na kutetemeka kila dakika, na kukustaajabia,

Sasa visiwa vitatetemeka katika siku ya kuanguka kwako; naam, visiwa vilivyo katika bahari vitafadhaika, kwa sababu ya kuondoka kwako.

Nami nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu, na kuzifanya nyota zake kuwa giza; nami nitalifunika jua kwa wingu, wala mwezi hautatoa nuru yake.

Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za BWANA, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.