Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arubaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.
Ezekieli 30:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao watakuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake itakuwamo kati ya miji iliyoharibika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Misri itakuwa jangwa kama nchi zilizo jangwa na miji yake itakuwa magofu kama miji iliyoteketezwa. Biblia Habari Njema - BHND Misri itakuwa jangwa kama nchi zilizo jangwa na miji yake itakuwa magofu kama miji iliyoteketezwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Misri itakuwa jangwa kama nchi zilizo jangwa na miji yake itakuwa magofu kama miji iliyoteketezwa. Neno: Bibilia Takatifu Hizo nchi zitakua ukiwa miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yao itakuwa magofu miongoni mwa miji iliyo magofu. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yao itakuwa magofu miongoni mwa miji iliyo magofu. BIBLIA KISWAHILI Nao watakuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake itakuwamo kati ya miji iliyoharibika. |
Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arubaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.
Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami nimeufanya.