Basi mfalme wa Misri hakuja tena kutoka nchi yake; kwa kuwa mfalme wa Babeli alikuwa amemnyang'anya nchi, tangu kijito cha Misri mpaka mto wa Frati, yote aliyokuwa nayo mfalme wa Misri.
Ezekieli 30:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri, na tazama, haukufungwa ili kuutia dawa, haukuzongwa kwa kitambaa, upate kuwa na nguvu za kushika upanga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wewe mtu! Nimeuvunja mkono wa Farao mfalme wa Misri, nao haukufungwa ili uweze kupona na kuweza kushika upanga. Biblia Habari Njema - BHND “Wewe mtu! Nimeuvunja mkono wa Farao mfalme wa Misri, nao haukufungwa ili uweze kupona na kuweza kushika upanga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Wewe mtu! Nimeuvunja mkono wa Farao mfalme wa Misri, nao haukufungwa ili uweze kupona na kuweza kushika upanga. Neno: Bibilia Takatifu “Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga. Neno: Maandiko Matakatifu “Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga. BIBLIA KISWAHILI Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri, na tazama, haukufungwa ili kuutia dawa, haukuzongwa kwa kitambaa, upate kuwa na nguvu za kushika upanga. |
Basi mfalme wa Misri hakuja tena kutoka nchi yake; kwa kuwa mfalme wa Babeli alikuwa amemnyang'anya nchi, tangu kijito cha Misri mpaka mto wa Frati, yote aliyokuwa nayo mfalme wa Misri.
Toka wayo wa mguu hadi kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwazongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.
BWANA asema hivi, Tazama, nitamtia Farao Hofra, mfalme wa Misri, katika mikono ya adui zake, na katika mikono yao wamtafutao roho yake; kama vile nilivyomtia Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, adui yake aliyeitafuta roho yake.
Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.
Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema BWANA. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya BWANA
Nami nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, na kuutia upanga wangu katika mkono wake, bali mikono ya Farao nitaivunja, naye ataugua mbele yake, kwa mauguzi ya mtu aliyetiwa jeraha la kumwua.
nami nitaupiga upinde wako, utoke katika mkono wako wa kushoto, na mishale yako nitaiangusha, itoke katika mkono wako wa kulia.
Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni; tunutu huharibu; kisha huruka juu na kwenda zake.
Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kulia; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kulia litakuwa limepofuka.
Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.