Ezekieli 30:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hivyo ndivyo nitakavyotekeleza hukumu katika Misri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndivyo nitakavyoiadhibu Misri. Na watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema - BHND Ndivyo nitakavyoiadhibu Misri. Na watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndivyo nitakavyoiadhibu Misri. Na watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu, nao watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu, nao watajua kuwa Mimi ndimi bwana.’ ” BIBLIA KISWAHILI Hivyo ndivyo nitakavyotekeleza hukumu katika Misri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. |
useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee Sidoni, nami natukuzwa kati yako; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu ndani yake, na kutakasika ndani yake.
Nami nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa, nami nitatia moto katika Soani, nami nitatekeleza hukumu katika No.
Nitakapoifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa na jangwa, nchi iliyopungukiwa na vitu vilivyoijaza, nitakapowapiga watu wote wakaao ndani yake, ndipo watakapojua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Nami nitauweka utukufu wangu kati ya mataifa, na mataifa wote wataiona hukumu yangu niliyoitekeleza, na mkono wangu niliouweka juu yao.
Nayo itakuwa tukano na aibu, na mafundisho na ajabu, kwa mataifa wakuzungukao, hapo nitakapotekeleza hukumu ndani yako, kwa hasira, na kwa ghadhabu, na kwa adhabu kali; mimi, BWANA, nimeyanena hayo;
basi, Bwana MUNGU asema hivi; Angalia, mimi, naam, mimi, ni juu yako; nami nitafanya hukumu kati yako machoni pa mataifa.
hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo.
Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,
Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;