Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe. Na Yusufu akaenda huku na huko katika nchi yote ya Misri.
Ezekieli 30:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Vijana wa Oni, na wa Pi-besethi, wataanguka kwa upanga; na miji hiyo itakwenda utumwani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Vijana wanaume wa Oni na Pi-besethi watauawa kwa upanga, na wakazi wengine watachukuliwa uhamishoni. Biblia Habari Njema - BHND Vijana wanaume wa Oni na Pi-besethi watauawa kwa upanga, na wakazi wengine watachukuliwa uhamishoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Vijana wanaume wa Oni na Pi-besethi watauawa kwa upanga, na wakazi wengine watachukuliwa uhamishoni. Neno: Bibilia Takatifu Wanaume vijana wa Oni na wa Pi-Besethi wataanguka kwa upanga nayo hiyo miji itatekwa. Neno: Maandiko Matakatifu Wanaume vijana wa Oni na wa Pi-Besethi wataanguka kwa upanga nayo hiyo miji itatekwa. BIBLIA KISWAHILI Vijana wa Oni, na wa Pi-besethi, wataanguka kwa upanga; na miji hiyo itakwenda utumwani. |
Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe. Na Yusufu akaenda huku na huko katika nchi yote ya Misri.
Walizaliwa kwake Yusufu katika nchi ya Misri, Manase na Efraimu, aliomzalia Asenathi binti Potifera, kuhani wa Oni.
Naye atazivunja nguzo za Beth-shemeshi, iliyoko huko katika nchi ya Misri, na nyumba za miungu ya Misri ataziteketeza.
Nami nitatia moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, na No itavunjika kabisa; na Nofu itakuwa na adui wakati wa mchana.
Nami nitalivunja komeo la Dameski, na kuwakatilia mbali wenyeji wa bondeni mwa Aveni, na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Beth-Adini; na watu wa Shamu watakwenda uhamishoni hadi Kiri, asema BWANA.