Ezekieli 30:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nami nitaikausha mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi, BWANA, nimenena neno hili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitaukausha mto Nili na vijito vyake, na kuwauzia watu waovu nchi ya Misri. Nitasababisha uharibifu nchini kote kwa mkono wa watu wageni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema - BHND Nitaukausha mto Nili na vijito vyake, na kuwauzia watu waovu nchi ya Misri. Nitasababisha uharibifu nchini kote kwa mkono wa watu wageni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitaukausha mto Nili na vijito vyake, na kuwauzia watu waovu nchi ya Misri. Nitasababisha uharibifu nchini kote kwa mkono wa watu wageni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Neno: Bibilia Takatifu Nitakausha vijito vya Mto Naili, na kuiuza nchi kwa watu waovu; kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilicho ndani yake. Mimi Mwenyezi Mungu nimenena haya. Neno: Maandiko Matakatifu Nitakausha vijito vya Naili na nitaiuza nchi kwa watu waovu, kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilichomo ndani yake. Mimi bwana nimenena haya. BIBLIA KISWAHILI Nami nitaikausha mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi, BWANA, nimenena neno hili. |
Ukosefu wa mvua uko juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu.
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu.
Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.
nena, useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa aoteaye kati ya mito yake, aliyesema, Mto wangu ni wangu mwenyewe, nami nimeufanya kwa ajili ya nafsi yangu.
Na wageni, watu wa mataifa watishao, wamemkatilia mbali na kumwacha; juu ya milima na katika mabonde yote matawi yake yameanguka, na vitanzu vyake vimevunjika karibu na mifereji yote ya nchi; na watu wote wa dunia wameshuka, wakitoka katika uvuli wake na kumwacha.
Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote; Bashani hulegea, na Karmeli; nalo ua la Lebanoni hulegea.
Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.