Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Ezekieli 30:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Yeye, na watu wake pamoja naye, watu wa mataifa watishao, wataletwa waingie katika nchi waiharibu, nao watafuta panga zao wapigane na Misri, na kuijaza nchi wale waliouawa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Nebukadneza mwenyewe pamoja na watu wake, taifa katili kuliko mataifa yote, watatumwa kuiangamiza nchi ya Misri. Watachomoa panga zao dhidi ya Misri na kuijaza nchi hiyo watu waliouawa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Nebukadneza mwenyewe pamoja na watu wake, taifa katili kuliko mataifa yote, watatumwa kuiangamiza nchi ya Misri. Watachomoa panga zao dhidi ya Misri na kuijaza nchi hiyo watu waliouawa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Nebukadneza mwenyewe pamoja na watu wake, taifa katili kuliko mataifa yote, watatumwa kuiangamiza nchi ya Misri. Watachomoa panga zao dhidi ya Misri na kuijaza nchi hiyo watu waliouawa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote, ataletwa ili kuangamiza nchi. Watafuta panga zao dhidi ya Misri na kuijaza nchi kwa waliouawa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote, litaletwa ili kuangamiza nchi. Watafuta panga zao dhidi ya Misri na kuijaza nchi kwa waliouawa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Yeye, na watu wake pamoja naye, watu wa mataifa watishao, wataletwa waingie katika nchi waiharibu, nao watafuta panga zao wapigane na Misri, na kuijaza nchi wale waliouawa.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Ezekieli 30:11
14 Marejeleo ya Msalaba  

basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako.

Nami nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, na kuutia upanga wangu katika mkono wake, bali mikono ya Farao nitaivunja, naye ataugua mbele yake, kwa mauguzi ya mtu aliyetiwa jeraha la kumwua.

mimi nitamtia katika mikono yake aliye mkuu kati ya mataifa; naye atamtenda mambo; nimemfukuza kwa sababu ya uovu wake.

Na wageni, watu wa mataifa watishao, wamemkatilia mbali na kumwacha; juu ya milima na katika mabonde yote matawi yake yameanguka, na vitanzu vyake vimevunjika karibu na mifereji yote ya nchi; na watu wote wa dunia wameshuka, wakitoka katika uvuli wake na kumwacha.

Kwa panga za mashujaa nitawaangusha watu wako umati wote; hao wote ni watu wa mataifa watishao, nao watakiharibu kiburi cha Misri, na jamii ya watu wake wengi wataangamia.

Nami nitaijaza milima yake watu wake waliouawa; katika milima yako, na katika mabonde yako, na mito yako yote, wataanguka wao watakaouawa kwa upanga.

Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa pori, uliwe na wao.

taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana;