Naye atakuja, na kuipiga nchi ya Misri; watu walioandikiwa kufa watakufa, nao walioandikiwa kuwa mateka watakuwa mateka, nao walioandikiwa kupigwa kwa upanga watapigwa kwa upanga.
Ezekieli 30:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaukomesha wingi wa watu wa Misri, kwa mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitamtumia Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, kukomesha utajiri wa nchi ya Misri. Biblia Habari Njema - BHND “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitamtumia Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, kukomesha utajiri wa nchi ya Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitamtumia Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, kukomesha utajiri wa nchi ya Misri. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “ ‘Nitakomesha makundi ya Misri kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. BIBLIA KISWAHILI Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaukomesha wingi wa watu wa Misri, kwa mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli. |
Naye atakuja, na kuipiga nchi ya Misri; watu walioandikiwa kufa watakufa, nao walioandikiwa kuwa mateka watakuwa mateka, nao walioandikiwa kupigwa kwa upanga watapigwa kwa upanga.
basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako.
Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitampa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hiyo nchi ya Misri; naye atawachukua watu wake jamii yote pia, na kutwaa mateka yake, na kutwaa mawindo yake, nayo yatakuwa ndio mshahara wa jeshi lake.
mimi nitamtia katika mikono yake aliye mkuu kati ya mataifa; naye atamtenda mambo; nimemfukuza kwa sababu ya uovu wake.
Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri, na jamii ya watu wake, Je! Umefanana na nani katika ukuu wako?