Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua niliyasikia.
Ezekieli 3:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana wewe hukutumwa kwa watu wa lugha isiyoeleweka, ama wa lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikutumi kwa taifa lenye lugha ngeni na ngumu, bali kwa Waisraeli. Biblia Habari Njema - BHND Sikutumi kwa taifa lenye lugha ngeni na ngumu, bali kwa Waisraeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikutumi kwa taifa lenye lugha ngeni na ngumu, bali kwa Waisraeli. Neno: Bibilia Takatifu Hukutumwa kwa taifa lenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Hukutumwa kwa taifa lenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli. BIBLIA KISWAHILI Maana wewe hukutumwa kwa watu wa lugha isiyoeleweka, ama wa lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli; |
Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua niliyasikia.
Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuielewa.
si kwa watu wa kabila nyingi wenye usemi usioeleweka, na lugha ngumu, ambao huwezi kufahamu maneno yao. Bila shaka, kama ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza.
Kisha Roho ikaniinua, ikanichukua mpaka katika ua wa ndani; na tazama, utukufu wa BWANA uliijaza nyumba.
Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa lugha ya Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.