Sasa tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo mtu akiitegemea, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.
Ezekieli 29:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na watu wote wakaao Misri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, kwa sababu wamekuwa mwanzi wa kutegemewa kwa nyumba ya Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo ndipo wakazi wote wa Misri watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. “Waisraeli walikutegemea wewe ee Misri, lakini umekuwa dhaifu kama utete. Biblia Habari Njema - BHND Hapo ndipo wakazi wote wa Misri watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. “Waisraeli walikutegemea wewe ee Misri, lakini umekuwa dhaifu kama utete. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo ndipo wakazi wote wa Misri watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. “Waisraeli walikutegemea wewe ee Misri, lakini umekuwa dhaifu kama utete. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo wale wote wanaoishi Misri watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. “ ‘Umekuwa fimbo ya tete kwa nyumba ya Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo wale wote waishio Misri watakapojua kuwa Mimi ndimi bwana. “ ‘Umekuwa fimbo ya tete kwa nyumba ya Israeli. BIBLIA KISWAHILI Na watu wote wakaao Misri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, kwa sababu wamekuwa mwanzi wa kutegemewa kwa nyumba ya Israeli. |
Sasa tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo mtu akiitegemea, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.
Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa ofisa mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi?
Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi wake.
Kwani wakati huu nitaleta mapigo yangu yote juu ya moyo wako, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako; ili upate kujua ya kuwa hapana mmoja mfano wa mimi ulimwenguni kote.
Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliovunjika, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.
Mbona unatangatanga hivi upate kugeuza mwendo wako? Utaona haya kwa ajili ya Misri pia, kama ulivyoona haya kwa ajili ya Ashuru.
Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa.
Wala Farao na jeshi lake kubwa, na kusanyiko lake kuu la watu, hawatamfaa kitu vitani, watakapofanya maboma, na kujenga ngome, ili kukatilia mbali watu wengi.
Nao watakaa humo salama; naam, watajenga nyumba, na kupanda mashamba ya mizabibu, na kukaa salama; nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu juu ya watu wote, wanaowatenda mambo ya jeuri pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao.
Wala hautakuwa tena tegemeo la nyumba ya Israeli, kufanya maovu yakumbukwe, watakapogeuka kuangalia nyuma yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoweka moto katika Misri, na hao wote wamsaidiao watakapoangamia.