Ezekieli 29:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Utakuwa duni kuliko falme zote; wala hautajiinua tena juu ya mataifa; nami nitawapunguza, ili wasitawale tena juu ya mataifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ufalme dhaifu kuliko falme zote; wala hawataweza kujikuza juu ya mataifa mengine. Nitawafanya Wamisri wawe watu dhaifu hata wasiweze kuyatawala mataifa mengine tena. Biblia Habari Njema - BHND ufalme dhaifu kuliko falme zote; wala hawataweza kujikuza juu ya mataifa mengine. Nitawafanya Wamisri wawe watu dhaifu hata wasiweze kuyatawala mataifa mengine tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ufalme dhaifu kuliko falme zote; wala hawataweza kujikuza juu ya mataifa mengine. Nitawafanya Wamisri wawe watu dhaifu hata wasiweze kuyatawala mataifa mengine tena. Neno: Bibilia Takatifu Utakuwa ufalme dhaifu kuliko zote na kamwe Misri haitajikweza tena juu ya mataifa mengine. Nitaufanya ufalme wake dhaifu sana kiasi kwamba kamwe hautatawala tena juu ya mataifa mengine. Neno: Maandiko Matakatifu Utakuwa ufalme dhaifu kuliko zote na kamwe Misri haitajikweza tena juu ya mataifa mengine. Nitaufanya ufalme wake dhaifu sana kiasi kwamba kamwe hautatawala tena juu ya mataifa mengine. BIBLIA KISWAHILI Utakuwa duni kuliko falme zote; wala hautajiinua tena juu ya mataifa; nami nitawapunguza, ili wasitawale tena juu ya mataifa. |
Ikakua, ikawa mzabibu wenye kuenea sana, wa kimo kifupi, ambao matawi yake yalimgeukia, na mizizi yake ilikuwa chini yake; basi ukawa mzabibu, ukatoa matawi, ukachipuza vichipuko.
Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu, wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri, nami nitatia hofu katika nchi ya Misri.
Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri, na jamii ya watu wake, Je! Umefanana na nani katika ukuu wako?
Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwanasimba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.
Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.