Ndipo Hiramu, mfalme wa Tiro, akawatuma watumishi wake kwa Sulemani; kwani alikuwa amesikia ya kwamba wamemtia mafuta awe mfalme mahali pa baba yake. Kwa maana Hiramu alikuwa akimpenda Daudi siku zote.
Ezekieli 27:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mbao zako zote wamezifanya kwa misonobari itokayo Seniri; wametwaa mierezi ya Lebanoni ili kukufanyia mlingoti; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wajenzi wako walitumia misonobari kutoka Seniri kupasua mbao zako zote; walichukua mierezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti. Biblia Habari Njema - BHND Wajenzi wako walitumia misonobari kutoka Seniri kupasua mbao zako zote; walichukua mierezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wajenzi wako walitumia misonobari kutoka Seniri kupasua mbao zako zote; walichukua mierezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti. Neno: Bibilia Takatifu Walizifanya mbao zako zote kwa misunobari kutoka Seniri; walichukua mwerezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti. Neno: Maandiko Matakatifu Walizifanya mbao zako zote kwa misunobari itokayo Seniri; walichukua mierezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti. BIBLIA KISWAHILI Mbao zako zote wamezifanya kwa misonobari itokayo Seniri; wametwaa mierezi ya Lebanoni ili kukufanyia mlingoti; |
Ndipo Hiramu, mfalme wa Tiro, akawatuma watumishi wake kwa Sulemani; kwani alikuwa amesikia ya kwamba wamemtia mafuta awe mfalme mahali pa baba yake. Kwa maana Hiramu alikuwa akimpenda Daudi siku zote.
Basi uamuru wanikatie mierezi ya Lebanoni; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni.
Na wana wa nusu kabila la Manase walikaa katika nchi; nao wakaongezeka kutoka Bashani mpaka Baal-hermoni, na Seniri, na mlima Hermoni.
Unitumie mtu stadi wa kuchonga dhahabu, fedha, shaba na chuma, na wa nguo za urujuani, nyekundu na samawati, ajuaye kutia nakshi, awe mmoja wa mastadi walioko pamoja nami Yuda na Yerusalemu ambao aliwaweka baba yangu Daudi.
Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni, Pamoja nami toka Lebanoni. Shuka kutoka kilele cha Amana, Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni; Kutoka mapangoni mwa simba, Kutoka milimani mwa chui.
Naam, misonobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia.