Ezekieli 27:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Merikebu za Tarshishi zilikuwa misafara yako, kwa bidhaa yako; nawe ulijazwa sana, ukawa mtukufu sana, katika moyo wa bahari. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Merikebu za Tarshishi ndizo zilikusafirishia bidhaa zako. Basi kama meli katikati ya bahari wewe ulikuwa umejaa shehena. Biblia Habari Njema - BHND Merikebu za Tarshishi ndizo zilikusafirishia bidhaa zako. Basi kama meli katikati ya bahari wewe ulikuwa umejaa shehena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Merikebu za Tarshishi ndizo zilikusafirishia bidhaa zako. Basi kama meli katikati ya bahari wewe ulikuwa umejaa shehena. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Merikebu za Tarshishi ndizo zinazokusafirishia bidhaa zako. Umejazwa shehena kubwa katika moyo wa bahari. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Merikebu za Tarshishi ndizo zinazokusafirishia bidhaa zako. Umejazwa shehena kubwa katika moyo wa bahari. BIBLIA KISWAHILI Merikebu za Tarshishi zilikuwa misafara yako, kwa bidhaa yako; nawe ulijazwa sana, ukawa mtukufu sana, katika moyo wa bahari. |
Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.
Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe.
Hao ndio waliokuwa wachuuzi wako, kwa vitu vya tunu, kwa vitumba vya nguo za samawati na kazi ya taraza, na masanduku ya mavazi ya thamani, yaliyofungwa kwa kamba, na kufanyizwa kwa mti wa mierezi, katika bidhaa yako.